IQNA

Mkutano wa Mfumo wa Kiislamu wa Kibenki na Kifedha Afrika kufanyika Dar

18:57 - July 02, 2021
Habari ID: 3474062
TEHRAN (IQNA)- Mkutano wa Saba wa Mfumo wa Kiislamu wa Kifedha na Kibenki barani Afrika umepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Tanzania, Dar- es- Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa, zaidi ya wazungumzaji 15 wa kimataifa watatoa mchango wao kwa mada zinazojadiliwa.

Sekta ya benki na fedha ya Tanzania na nchi kadhaa za Afrika zitashiriki kikamilifu katika mkutano huo kupata maarifa ya kutosha juu ya sekta ya kifedha ya Kiislamu na suluhisho la shida zinazoongezeka za jamii.

Hafla hiyo imeandaliwa na AlHuda Centre of Islamic Banking and Economics (CIBE) na imedhaminiwa na Teknolojia ya ICD na Codebase, na inasaidiwa na SPM Consulting, CIFCA, na chuo cha London School of Modern Studies..

Washiriki wa ngazi za  juu kutoka nchi zaidi ya 20 wanatarajiwa kushiriki n.k. kutoka benki kuu, sekta za benki na fedha za Tanzania na nchi zingine za Kiafrika, na tasnia ya bima. Bwana M. Zubair Mughal, Afisa Mtendaji Mkuu wa AlHuda CIBE ameshukuru wafuasi na wafadhili kwa imani yao endelevu kwao na msaada mkubwa katika kuandaa kikao hicho.

Tanzania ina idadi kubwa ya watu wa vijijini, ambayo inafanya upatikanaji wa huduma za kifedha kuwa changamoto na suluhisho za dijiti kuwa bora.

Kuwekeza katika benki za Kiislam na fedha kunaweza kumaanisha uwekezaji mkubwa wa moja kwa moja wa kigeni (FDIs) ambao unaweza kuboresha ajira, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na kupunguza umaskini.

Malengo makuu ya mkutano huo ni pamoja na kutambua maendeleo makubwa katika Miundombinu ya kifedha ya Kiislamu, uhusiano wa tasnia ya fedha ya Kiislamu ya Afrika kwa masoko ya kifedha ya kimataifa, kuonyesha mabadiliko ya masoko ya kifedha ya Kiisilamu wakati wa mgogoro wa kifedha , kujadili mbinu bora zinazopaswa kutumiwa  mfumo wa kifedha wa Kiislamu , kutathmini ubunifu katika masoko ya kifedha ya Kiislamu kupitia bidhaa mpya zilizotengenezwa kwa utafiti, nk.

Hafla hiyo iko wazi kwa umma na ada ndogo itatozwa kwa washiriki. Inashauriwa sana kwamba wawakilishi wa mashirika, makampuni, na mabenki wajiunge na mkutano huo ili kupata faida kubwa katika mkutano huu wa kimataifa nchini Tanzania.

3981436/

Kishikizo: kifedha kiislamu benki
captcha