IQNA

Viongozi wanamapambano wa Palestina wampigia simu rais mteule wa Iran

12:32 - July 14, 2021
Habari ID: 3474098
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) Ismail Haniya na Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina Ziad al Nakhala wamempongeza rais mteule wa Iran Sayyid Ebrahim Raeisi kwa ushindi wake katika uchaguzi wa rais.

Katika mazungumzo ya simu nyakati tafauti, Haniya na Nakhala wameelekeza matumaini yao kuwa Raeisi atafanikiwa katika kipindi chake cha urais. Aidha wameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina.

Haniya ametoa ufafanuzi kuhusu ushindi wa hivi karibuni wa harakati za ukombozi wa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni huku akisisitiza kuhusu kuimarishwa uhusiano baina ya Hamas na Iran.

Naye rais mteule wa Iran wamewapongeza watu wa Palestina kwa ushindi wao  huku akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuunga mkono ukombozi wa Quds (Jerusalem). Aidha  Raeisi amelaani vikali kuendelezwa mzingiro dhidi ya Ukanda wa Ghaza.

3983972

 

captcha