Kwa mujibu wa taarifa miongoni mwa watakaoshiriki mashindano hayyo kuna maqarii, maimamu waadhini na wafanyakazi wa vituo vya kidini.
Awamu ya kwanza ya mashindano hayo itafanyika katika vituo vya wizara hiyo mikoani na kisha fainali itafanyika Cairo katika jengo la Wizara ya Wakfu.
Kila mwaka wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Misri hutuma wasomaji Qur’ani na wahubiri katika nchi mbali mbali duniani.
Wamisri ni maarufu kwa usomaji Qur'ani na hadi sasa kuna wasomaji au maqarii wengi wa Qur'ani kutoka nchi hiyo ambayo wamepata umashuhuri duniani na miongoni mwa walivuma zaidi ni marhum Sheikh Abdul-Basit Abdus-Samad.