IQNA

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’an ya Meshkat

12:01 - February 28, 2022
Habari ID: 3474985
TEHRAN (IQNA) – Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Meshkat wametangazwa baada ya klipu zao kusikilizwa na jopo la majaji.

Hujjatul  Islam Mujtaba Muhammadi, Mkurugenzi wa Taasisi ya Qur’ani ya Meshkat amewataja washindi kuwa Jalil Ashrafi, Ali Akbar Basaeri, Mohammad Javad Golchin, Ahmad Hosseini, Mostfa Savari, Ali Reza Makkari, Akbar Mehdi Josheqani, Mohammad Javad Hashemi, na Ami Yunesi kutoka Iran, Jomaa Abdul Ghani wa Nigeria na Seyed Amir Hashemi kutoka Afghanistan.

Amesema washindi watatangazwa katika sherehe siku ya Jumatano.

Mashindano hayo yatafanyikwa kukiwa na hadhirina wachache kutokana na janga la COVID-19 na kuongeza kuwa sherehe hizo zitarushwa mubashara kupitia TV ya Qur’ani na Radio ya Qur’ani nchini Iran.

Hujjatul Islam Muhammadi amesema watu 4,000 kutoka Iran na maeneo mengine duniani wameshiriki katika mashindano hayo ambayo yamefanyika kwa njia ya intaneti.

Mashindano hayo yanalenga kustawisha harakati za Qur’ani na kuimarisha ufahamu wa Qur’ani katika jamii, amesema Hujjatul  Islam Mujtaba Muhammadi.

4039145

captcha