IQNA

Mbunge wa Palestina: Israel haiwezi kubadilishwa kwa kuiba ardhi

20:48 - March 04, 2022
Habari ID: 3475005
TEHRAN (IQNA) - Mbunge wa Palestina anasema hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuiba ardhi ya Wapalestina huko Quds (Jerusalem) haibadilishi ukweli wa mambo.

Ahmad Attoun aliyasema hayo Jumatano baada ya Kamati ya Mipango na Ujenzi ya utawala wa Kizayuni kuamua kuiba ardhi ya makaburi ya Waislamu ya karne nyingi yajulikanayo kama Makaburi ya Al-Yusufiyah yaliyoko mashariki mwa Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds.

Mbunge huyo, alisema kuwa kitendo cha Israel kuiba ardhi hiyo kinaonyesha kuendelea kwa utawala huo "kuyahudisha Mji Mkongwe wa Jerusalem na kubadili utambulisho wake."

"Hii njama iliyoratibiwa  kimfumo iliyopitishwa kuyahudisha Mji Mtakatifu, kulazimisha misimamo ya Israeli na kuhujumu turathi za Kiislamu za Palestina na nembo za ustaarabu wake," aliongeza mbunge huyo ambaye amefukuzwa kutoka Al-Quds.

Attoun alisema kuwa kufanya kuhujumu makaburi ya Al-Yusufiyah na kufukua makaburi yake mbele ya macho ya ulimwengu huku kila mtu akikaa kimya "ni jambo la kutisha."

Mbunge huyo wa Palestina alitoa wito wa kuchukuliwa hatua za kivitendo kote katika ardhi za Palestina na ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu dhidi ya hatua ya Israel.

Amesisitiza kuwa uvamizi wa Israel hautaweza kufuta turathi za Wapalestina mjini Quds "kwa sababu Quds ni sehemu ya imani yetu."

3478024

captcha