IQNA

Sala ya Tahajud yaruhusiwa katika Misikiti Misri siku za mwisho za Ramadhani

17:33 - April 26, 2022
Habari ID: 3475171
TEHRAN (IQNA) – Misikiti mikubwa nchini Misri itaruhusiwa kufanya misa ya usiku wa manane katika siku za mwisho za Ramadhani.

Wizara ya Awqaf (Wakfu)  ya Misri ilibatilisha uamuzi wa hapo awali uliotolewa Aprili 15 wa kupiga marufuku sala ya usiku ya Tahajud mwaka huu ikitaja wasiwasi wa corona.

Hatahivyo uamuzi huo utaruhusu sala ya Tahajud kusaliwa tu katika misikiti mikubwa nchini Misri pekee.

Katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Sala ya Tahajud (sala ya Usiku isiyo ya faradhi) kwa kawaida huswaliwa usiku baada ya Sala ya Tarawehe katika siku kumi za mwisho za mwezi huu mtukufu.

Wizara ya Wakfu ya Misri pia imeruhusu  mihadhara maalum ya Ramadhani katika misikiti ya nchi hiyo baada ya kusitishwa kwa miaka miwili (kutoka Machi 19, 2020), mradi hatua za kuzuia maambukizi ya corona zichukuliwe

Huku swala ya Tarawehe ikiendelea kuswaliwa misikitini ikiwa ni tahadhari, Waziri wa Wakfu wa Misri pia amewaruhusu wanawake kushiriki katika sala hiyo tena.

Hapo awali serikali ya Misri ilitangaza uamuzi wake wa kuruhusu kuanzishwa tena kwa Iftar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

/3478654

captcha