IQNA

Watoto na Qur'ani

Al- Azhar yatetea mpango wa darsa za watoto za kuhifadhi Qur'ani

17:54 - May 30, 2022
Habari ID: 3475316
TEHRAN (IQNA)-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimejibu ukosoaji kuhusu darsa zake za kuhifadhi Qur'ani kwa watoto. Katika taarifa yake Jumapili, Kituo cha Al-Azhar cha Fatwa za Kielektroniki kilisema kuwa kulea watoto na kuwalea kwa ufahamu sahihi wa Quran ni nguzo ya utulivu wa jamii.

“Kuwalea watoto wetu kukielewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kukihifadhi, kukisoma, na kufuata mafunzo yake na hivyo kusaidia katika malezi yao mema, kulinda fitra yao, na utakasifu wa ubinadamu wao, kuwapa ufahamu Qur'ani wenye nuru na muelekeo wa wastani,” ilisema taarifa ya Facebook ya kituo hicho.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Aidha, Qur'ani Tukufu inasaidia katika kufahamu lugha yetu ya Kiarabu, sarufi yake, matamshi yake, ubunifu na uboreshaji wake."

Kauli hiyo ilikuja baada ya mkosoaji wa Misri Salwa Bakr kukosoa masomo ya kuhifadhi Quran kwa watoto nchini Misri, akidai kuwa darsa hizi zinawanyima watoto utoto wao. Matamshi hayo yalizua hisia kwenye mitandao ya kijamii nchini Misri huku baadhi ya wanaharakati na wataalamu wakikataa madai yake kama na kumtuhumu kuwa "ametia chumvi".

Al Azhar imesema wito wa kuwaweka vijana mbali na Qur'ani Tukufu na mafundisho yake matukufu ni wito wa wazi wa kuwaweka mbali na dini yao, maadili yao, na kuwatenga na lugha na utamaduni wao, na utambulisho wao, mbali na kuwa wito kama huo unafungua mlango wa mawazo ya uharibifu na tafsiri potovu.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Qur'ani Tukufu imeweka misingi ya uhuru na heshima kwa dini na imetoa wito wa udugu na usawa wa binadamu bila ya ubaguzi wa dini, rangi, na lugha.

Hapana shaka kwamba ufahamu sahihi na wenye nidhamu wa Qur'ani Tukufu ndiyo njia muhimu zaidi ya kuishi pamoja kwa amani, kukubalika kwa wengine, na kuwa mfuasi mzuri wa usalama na utulivu wa jamii, imesema taarifa ya Al Azhar.

 4060650

captcha