IQNA

Imam Ridha AS

Bendera ya Imam Ridha AS yapokewa kwa furaha na Waislamu wa Tanzania +Video

15:41 - June 13, 2022
Habari ID: 3475372
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Tanzania wamepata fursa ya kuipokea kwa furaha bendera ya Imam Ridha AS ambayo ilikuwa katika msafara wa kimataifa wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa mtukufu huyo.

Idadi kubwa ya Waislamu wamejitokeza katika mji mkubwa zaidi wa Tanzania, Dar es Salaam kuipkea bendera hiyo ya Haram Takatifu ya Imam Ridha AS. Tanzania ni moja ya nchi zilizochagulia ambazo zinatembelewa na msafara wa 'Katika Kivuili cha Jua'ambao umetembelea nchi mbali mbali duniani baada ya kusitishwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na jgana la corona.

Waislamu waliojawa na furaha na raghba walijitokeza kuukarbisha msafara huo katika nchi hiyo ambao ulikuwa unaongoza na Rais wa Taasisi ya Karamat Razavi Bw. Mohammad Hassan Ostad Aghad na wahudumu kadhaa wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS.

Ikumbukwe kuwa, miaka 1295 iliyopita, sawa na tarehe 11 Dhulqaada mwaka 148 Hijria, alizaliwa Imam Ali bin Mussa Ridha AS, mmoja kati ya Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad AS katika mji wa Madina.

Idadi kubwa ya waumini wamefika katika haram hiyo kwa ajili ya kujumuika katika siku hii ya furaha ya kukumbuka kuzaliwa Imam Ali bin Musa Ridha AS ambaye ni kutoka katika kizazi kilichotakasika cha Mtume Muhammad SAW.

Imamu huyo mkarimu ambaye alikuwa mbeba bendera ya Wilaya, katika kipindi chote cha maisha yake yaliyojaa baraka aliufungulia Umma milango ya hekima na maarifa na hivyo akawa kigezo cha ucha Mungu na ubora kwa lengo la kufikia saada.

Haram Takatifu ya Imam Ridha AS iko katika mji wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

3479283

captcha