IQNA

Harakati za Qur'ani

Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani Yazinduliwa nchini Algeria

14:42 - October 19, 2022
Habari ID: 3475953
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 24 la Wiki ya Kitaifa ya Qur’ani limezinduliwa nchini Algeria katika sherehe siku ya Jumanne.

Waziri wa Masuala ya Kidini na Awqaf (Wakfu) Youcef Belmehdi alihudhuria hafla hiyo katika shule ya Qur'ani katika mji wa Beni Abbes magharibi mwa Algeria.

Katika hotuba yake, alisisitiza nafasi muhimu ya shule za Qur'ani katika kuwafundisha watoto Qur'ani na kuhifadhi utamaduni wa Kiislamu.

Alisema moja ya madhumuni ya kuanzisha na kuendeleza shule za Qur'ani ni kuwahimiza watoto katika ngazi za mitaa na kitaifa kuhifadhi Qur'ani na kuendeleza utamaduni wa Qur'ani katika familia.

Wiki ya Qur'ani ya kitaifa ya mwaka huu nchini Algeria inafanyika kwa kauli mbiu ya "Hijra (kuhama) katika Qur'ani Tukufu, Kujitolea kwa ajili ya Nchi, Kazi na Imani".

Kauli mbiu ya wiki ya kitaifa ya Qur'ani ya mwaka jana ilikuwa "Upendo kwa Nchi, Mwelekeo wa Maadili na Ahadi ya Kitaifa".

Jiji la Beni Abbes linaandaa hafla za wiki chini ya usimamizi ya wasomi wa vyuo vikuu na viongozi wa maombi.

Baadhi ya watu 200 kutoka mikoa mbalimbali ya nchi wanashiriki katika programu hizo.

Jiji hilo pia linaandaa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani kuhusu kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa makundi tofauti ya umri na katika kategoria mbalimbali.

Algeria ni nchi ya Kiarabu iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo.

4092873

Kishikizo: algeria wiki ya qurani
captcha