IQNA

Uislamu nchini Ujerumani

Uadui dhidi ya Uislamu unaongezeka Ujerumani Mashariki

11:28 - November 10, 2022
Habari ID: 3476064
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa utafiti, chuki dhidi ya wageni na chuki dhidi ya Waislamu imekuwa ikiongezeka kwa kasi mashariki mwa Ujerumani.

Takriban 46.6% ya watu mashariki mwa Ujerumani wanataka kupigwa marufuku kwa wahamiaji Waislamu, kutoka 40.2% ya watu mwaka 2020. Hayi ni kulingana na uchunguzi wa mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Leipzig uliochapishwa Jumatano.

Pia, 42.7% ya waliohojiwa walisema walijisikia kama wageni katika nchi yao kwa sababu ya idadi kubwa ya Waislamu.

Watafiti walisema kuwa mitazamo dhidi ya Uislamu ilikuwa juu katika majimbo ya zamani ya Ujerumani ya mashariki ya kikomunisti ambapo Waislamu wachache sana wanaishi na ambapo watu hawana mawasiliano mengi na Waislamu.

Magharibi mwa Ujerumani, 23.6% walisema wanatetea marufuku ya uhamiaji kutoka nchi za Kiislamu, na 36.6% walisema wanajisikia kama wageni katika nchi yao kutokana na idadi kubwa ya wahamiaji.

Utafiti wa 'Leipzig Authoritarianism 2022' pia umefichua kuwa chuki dhidi ya wageni ilikuwa inaongezeka katika majimbo ya mashariki ya Ujerumani.

Baadhi ya watu 33.1% waliohojiwa walikubaliana na kauli fulani za chuki dhidi ya wageni, huku wengi wao wakisema "Ujerumani imejaa wageni kwa kiwango hatari" na kwamba wanapaswa kutumwa katika nchi zao ikiwa kuna uhaba wa kazi nchini Ujerumani.

Nchi ya watu zaidi ya milioni 84, Ujerumani ina idadi ya pili kubywa ya Waislamu katika Ulaya Magharibi baada ya Ufaransa. Kuna Waislamu wapatao milioni 4.7 nchini humo, kulingana na takwimu rasmi.

Nchi hiyo imeshuhudia kuongezeka kwa ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu katika miaka ya hivi karibuni, ikichochewa na propaganda za vikundi na vyama vya mrengo mkali wa kulia, ambavyo vimetumia vibaya mzozo wa wakimbizi na kujaribu kuzua hofu kwa wahamiaji.

Mamlaka za Ujerumani zilisajili takriban uhalifu 662 wa chuki dhidi ya Uislamu mwaka 2021. Zaidi ya misikiti 46 ilishambuliwa kati ya Januari na Desemba mwaka jana na takriban watu 17 walijeruhiwa kutokana na ghasia dhidi ya Waislamu.

captcha