IQNA

Harakati za Qur’ani Misri

Vikao vya kujifunza Qur’ani kwa watoto katika Misikiti zaidi ya 6,000 nchini Misri

21:47 - December 16, 2022
Habari ID: 3476257
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Wakfu ya Misri imesema imeshaandaa vikao vya kufunza Qur'ani Tukufu maalumu kwa watoto katika zaidi ya misikiti 6,000 kote Misri.

Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema kuwa imetekeleza shughuli mbalimbali za Qur'ani nchini Misri tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Baadhi yao vikao hivyo vilihudhuriwa na wasomaji Qur’ani  wa viwango vya juu ambao walisoma Qur'ani kwa mbinu Warsh na Hafs, taarifa hiyo ilisema.

Vikao hivyo ya  Qur'ani vilipokelewa vyema na watu katika miji tofauti, wizara hiyo iliongeza.

Shughuli nyingine za Qur'ani zilizoandaliwa na Wizara ya Wakfi ni wiki 127  za kitamaduni katika misikiti, kozi za elimu katika nyanja za sayansi za Qur'ani na Hadithi, vikao vya Qur'ani kwa wanawake, na mafunzo  kwa maimamu wa misikiti, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Shughuli hizo zimekuwa na lengo la kukuza mafundisho ya Qur'ani Tukufu na Uislamu katika jamii, wizara hiyo iliendelea kusema.

Nchini Misri, Wizara ya Wakfu ina jukumu la kuandaa, kuratibu na kusimamia shughuli za Qur'ani na kidini.

 4107324

captcha