IQNA

Harakati za Qur'ani Kimataifa

Balozi: Iran, Malaysia kuendeleza 'Diplomasia ya Qur'ani Tukufu

19:03 - January 20, 2023
Habari ID: 3476435
TEHRAN (IQNA) - Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Malaysia amesema nchi hizo mbili zinatarajia kuendelea kutumia 'Diplomasia ya Qur'ani Tukufu' kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa pande hizo mbili.

"Iran na Malaysia ziko katika mchakato wa kuingia katika enzi mpya ya 'Diplomasia ya Qur'ani," Ali Asghar Mohammadi alimwambia ripota wa IQNA kando ya  Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Qur'ani la Restu  huko Putrajaya siku ya Ijumaa.

Matamshi hayo yanakuja wakati Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Malaysia kimekuwa mshirika katika kuandaa hafla hiyo. Iran pia imetuma ujumbe unaojumuisha wanaharakati wa Qur'ani katika sekta ya usanii kwenye hafla hiyo ili kuonyesha uwezo wa Iran.

Mwanadiplomasia huyo ameongeza kuwa, Iran ina uwezo mkubwa wa kushiriki katika matukio ya kimataifa ya Qur'ani, .

Juhudi zaidi zinahitajika ili kutambulisha kipengele cha kimataifa wanaharakati wa Qur'ani nchini Iran katika sekta ya usanii, alisema.

Quran Tukufu ni nguzo inayounganisha ulimwengu wa Kiislamu na tunapaswa kushikamana nayo, alisisitiza Mohammad.

Hafla hiyo inafanyika kwa lengo la kutilia maanani vipengele vipya vya masuala yanayohusiana na Qur'ani Tukufu na Wairani wana mengi ya kusema katika medani hii, alibainisha balozi huyo.

Hafla hiyo ilizinduliwa siku ya Ijumaa katika Nasyrul Quran Complex.

Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Qur'ani la Restu linafanyika Januari 20 hadi 29 huko Putrajaya, Malaysia, na waandaaji wametoa maelezo yake.

Hafla hiyo imeandaliwa na taasisi nyingi za Malaysia ikiwa ni pamoja na Wakfu wa Restu na washirika wa kigeni kama vile kituo cha kitamaduni cha Iran huko Malaysia na inafanyika katika Nasyrul Quran Complex huko Putrajaya.

Kulingana na kitabu cha programu kilichotolewa na waandaaji, hafla hiyo inawaruhusu wageni kushuhudia maonyesho maalum, na kuingiliana na wajasiriamali katika sekta za Qur'ani Tukufu na sanaa ya Kiislamu na bidhaa za Kiislamu huku pia wakijaribu kuboresha taswira ya Uislamu kama dini iliyojumuisha na ya amani.

Kuanzisha uhifadhi na ustawi wa Qur'ani Tukufu, kutukuza mafundisho ya Uislamu, kualika umma kupenda elimu na wanazuoni, kutumia teknolojia ya kisasa kama njia ya kuhubiri yenye ufanisi, na kujaribu kurudisha umma wa Kiislamu kwenye utambulisho wao wa kweli yametajwa miongoni mwa malengo mengine ya tamasha hilo.

3482141

captcha