IQNA

Jinai za Israel

Mufti wa Oman apinga ndege za Israel kuruhusiwa kutumia anga ya Oman

13:10 - February 26, 2023
Habari ID: 3476626
TEHRAN (IQNA)- Mufti wa Oman Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili ameitaka serikali ya nchi hiyo ibatilishe uamuzi wake wa kuruhusu anga yake kutumiwa na ndege za utawala haramu wa Israel.

Mufti Khalili ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwamba: Sisi tumeshangazwa mno na uamuzi huu wa kushtukiza ambao kwa hakika hatukutarajia.

Aidha Mufti Sheikh Khalili wa Oman ameongeza kuwa, sisi tulikuwa na matumaini kwamba, serikali yetu itaeandelea na misimamo ya kupinga kuanzisha uhusiano wa aina yoyote ile na utawala haramu wa Israel na ni kwa namna gani tulikuwa tukijifakharisha kwa hili.

Hayo yanajiri baada ya Eli Cohen Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Israel kudai kuwa, Oman imeidhinisha ndege za utawala huo haramu kuruka katika anga ya nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Oman bila kuitaja Israel kwa njia ya moja kwa moja, ilieandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa, anga ya nchi hiyo ya Kiarabu ipo wazi kwa ndege zote ambazo zimetimiza masharti na vigezo ilivyoweka.

Hii ni katika hali ambayo, Aprili mwaka jana 2022, Oman ilikataa kuidhinisha ndege za utawala wa haramu wa Israel kuruka katika anga yake, ikionekana kujiepusha kufuata nyayo za Saudi Arabia za kujikurubisha wazi wazi kwa utawala huo pandikizi.

Uamuzi huu ambao haukutarajiwa umewashangaza wengi hasa kutokana na kuwa, kwa muda mrefu sasa, Oman imekuwa ikisisitiza kuwa, haitakuwa na uhusiano wa kawaida na wa wazi na Israel hadi pale suala la Palestina litatatuliwa.

3482614

captcha