Wagombea 50 kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika walishiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani.
Ilijumuisha kategoria kadhaa za kuhifadhi Qur’ani Tukufu kwa kuzingatia sheria za Tajweed na Tartil.
Tawi la Ethiopia la Wakfu wa Mohammed VI wa Ulamaa wa Kiafrika limeandaa shindano hilo.
Washindi watashiriki katika hafla mashindano ya Qur'ani bara zima la Afrika ambayo yatahudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi kadhaa za Kiafrika.
Mashindano hayo yanalenga kukuza shughuli za Qur'ani na kuwahimiza vijana kujifunza na kutekeleza mafundisho ya Kiislamu.
Pia ni fursa ya kutambua vipaji na uwezo wa vijana katika nyanja za Qur'ani, kwa mujibu wa Mohammed al-Rafaqi, katibu mkuu wa Wakfu wa Mohammed VI wa Ulamaa wa Kiafrika
Wakfu wa Mohammed VI wa Ulamaa wa Kiafrika, kwa mujibu wa waanzilishi wake, ni taasisi ya kidini ya Kiislamu inayotaka kuzuia itikadi kali na kukabiliana na malumbano ya kimadhehebu baina ya Waislamu.
Lengo la msingi ni kuunganisha na kuratibu juhudi za wasomi wa Kiislamu kutoka Morocco na nchi nyingine za Afrika ili kuhimiza umoja na uvumilivu pamoja na utafiti wa kina wa mafunzo ya Kiislamu.
3482615