IQNA

Kadhia ya Quds Tukufu

Kongamani la dini mbali mbali lasisitiza ibada kwa waumini wote Quds Tukufu

16:32 - March 12, 2023
Habari ID: 3476696
TEHRAN (IQNA) – Kongamano la dini mbalimbali mjini Roma, Italia limesisitiza umuhimu wa uhuru wa kuabudu mjini al-Quds (Jeruslaem) kwa waumini wa dini za Kiislamu, Kikristo na Kiyahudi.

Wakati wa kongamano la Jumatano na Alhamisi iliyopita, Vatikani ilisisitiza umuhimu wa kuingia na kuabudu bila vizingiti katika maeneo yote matakatifu huko al-Quds.

Mkutano huo uliandaliwa na Kikundi Kazi cha Pamoja cha Mazungumzo Baina Dini Mbalimbali na Tume ya Palestina ya Mazungumzo ya Kidini.

Sheikh Mahmoud Al-Habbash, mshauri wa masuala ya kidini kwa Rais wa Mamlaka ya Palestina (PA) Mahmoud Abbas, aliongoza ujumbe wa PA.

Wajumbe mbalimbali walikutana mjini Vatican na Papa Francis, ambaye alihimiza juhudi za kikundi hiki cha kazi.

Katika taarifa yake, Ubalozi wa PA kwa Vatican ulisema kwamba karatasi za kitaaluma ziliwasilishwa wakati wa hafla hiyo zikirejelea: "Hali ya kiroho, kihistoria na kitamaduni ya mji wa Palestina kwa Waislamu na Wakristo."

Vatican News iliripoti kwamba Papa Francis pia: "Alisisitiza umuhimu wa kiroho wa al-Quds, ambayo iliunda mada iliyochaguliwa kwa mkutano wa kikundi kazi."

Alikariri wito alioutoa mwaka 2019 na mfalme wa Morocco, huku akitoa wito kwa al-Quds kuzingatiwa na kila mtu kama: "Urithi wa pamoja wa ubinadamu na haswa wafuasi wa dini tatu za tauhidi, kama mahali pa kukutana. na kama ishara ya kuishi pamoja kwa amani."

3482769

Kishikizo: quds tukufu palestina
captcha