IQNA

INM

Serikali ya Nigeria inakiuka haki za Sheikh Zakzaky, amenyimwa pasi ya kusafiria

19:20 - March 25, 2023
Habari ID: 3476757
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria (IMN) imekosoa kuendelea marufuku ya kusafiri iliyowekwa kwa kiongozi wake, Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Harakati hiyo ilisema hali ya kiafya ya mwanazuoni hiyo ilizorota akiwa kizuizini ndiyo sababu kuu ya kuanza kwa maandamano yake ya kila siku ya kutaka aachiliwe huru ambayo hufanyika  mjini Abuja.

Licha ya hukumu kadhaa za mahakama zilizoamuru kuachiliwa huru bila masharti Sheikh Zakzaky na mkewe Zeenah Ibrahim, serikali ya Nigeria imeendelea kukiuka haki zao kwa kuwawekea marufuku ya kusafiri na kuwanyang'anya hati zao za kusafiria za kimataifa.

Katika taarifa, Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imesema uamuzi wa Mahakama Kuu ya Kaduna iliyowaachia huru na kumuachilia huru Sheikh Zakzaky na mkewe iliwapa fursa ya kusafiri kwa ajili ya matibabu, ikisema hata hivyo serikali inawanyima pasi za kusafiria za kimataifa.

Taarifa hiyo ya Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imetiwa saini na Fatima Aliyu Adam wa Jukwaa la Kitaaluma la Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, " umma unapaswa kutambua kuwa Sheikh Zakzaky na mkewe wana changamoto nyingi za kiafya zinazohatarisha maisha kutokana na mauaji ya Zaria, na hadi sasa, kuna risasi nyingi katika miili yao. Amesema hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky na mkewe haihitaji tu wataalamu wa afya waliobobea bali pia kituo cha matibabu chenye vifaa vya kisasa.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake, Mallimah Zeenah walitiwa nguvuni tarehe 13 Disemba mwaka 2015 katika shambulizi lililofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya kituo cha kidini cha Baqiyyatullah katika mji wa Zaria na walikuwa mahabusu kwa kipindi cha miaka 6 iliyopita kabla ya kuachiliwa huru mwezi Julai mwaka 2021.

3482935

Kishikizo: nigeria zakzaky
captcha