IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Al-Kawthar TV: Waliofuzu nusu Fainali watajwa

17:58 - April 04, 2023
Habari ID: 3476810
TEHRAN (IQNA) – Maqarii kumi na wawili ambao wamefanikiwa kuingia katika raundi ya nusu fainali ya toleo la 16 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Televisheni ya Al-Kawthar.

Kwa mujibu wa jopo la waamuzi, Saeed Rahimi, Ali Reza Lotfinia, Mojtaba Harandizadeh, na Hamed Karmalakaab kutoka Iran, Ahmed Razzaq Al-Dalfi, Muhammad Zalif Atiya Wali, na Zia Badri Ahmed al-Mousawi kutoka Iraq, Abdul Razzaq Ashraf Al-Shahwi. , Ahmed Samir Abdul Aziz, na Muhammad Ibrahim Muhammad Ismail kutoka Misri, Ahmed Safi al-Halabi kutoka Syria, na Muhammad Ridha al-Aman Surtman kutoka Indonesia wamefuzu kwa nusu fainali.

Majina ya washiriki wengine kumi na wawili waliofuzu nusu fainali yatatangazwa katika siku zinazofuata.

Raundi ya nusu fainali itafanyika usiku wa 25 wa Ramadhani kwa kushirikisha wasomaji au maqarii 24 bora.

Hatimaye maqarii watano bora watashindana katika raundi ya mwisho usiku wa kabla ya Eid Al-Fitr.

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika kwa njia ya simu yamepewa anuani ya "Inna lil-Muttaqina Mafaza" (Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu- Quran Tukufu, Surat An Nabaa  aya ya 31) hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ni mashindano makubwa zaidi ya ulimwengu ya Kiislamu ya usomaji wa Qur'ani moja kwa moja kwa njia ya televisheni yanayorushwa na Al-Kawthar, Televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).

Wale wanaopenda wanaweza kutazama mashindano hayo wakati wa usiku kwenye Al-Kawthar TV au kupitia tovuti ya https://www.alkawthartv.ir/live

4131370

captcha