IQNA

Mashindano ya Qur''ani

Qari wa Misri ashinda katika Mashindano ya Qur'ani ya 'Awal Al Awail' Qatar

21:19 - November 13, 2023
Habari ID: 3477886
TEHRAN (IQNA) – Qari wa Misri ametwaa taji la toleo la pili la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya "Awal Al Awail" nchini Qatar.

Mashindano hayo ni sehemu ya kimataifa ya mashindano ya Qur'ani ya Sheikh Jassim bin Muhammad Al Thani, yaliyoandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar. Washiriki walishindana katika kategoria tofauti zinazojumuisha kuhifadhi Qur'ani, Tajweed, Tarteel na maana ya maneno ya Qur'ani

Mshindi, Muhammad Saad Abdul Jalil kutoka Misri, alitunukiwa na Waziri wa Awqaf na Masuala ya Kiislamu Ghanem bin Shaheen bin Ghanem Al Ghanim katika hafla ya kufunga iliyofanyika katika Hoteli ya Sheraton siku ya Jumapili. Alipokea ngao ya heshima, cheti cha shukrani, na zawadi ya riyal milioni moja za Qatar (karibu $250,000 USD), Al-Raya Daily iliripoti Jumatatu.

Kamati ya waamuzi inayoongozwa na Sheikh Ahmed Issa Al-Masarawi pia ilitunukiwa katika sherehe hizo. Shindano hilo lililochukua siku 12, lilishuhudiwa ushindani mkubwa kati ya washiriki 80 kutoka nchi 26.
Qari wa Misri, Muhammad Saad Abdel Jalil, ambaye alishinda taji la shindano hilo, alielezea furaha yake ya kupata taji hilo, lakini pia alikiri jukumu lililokuja nalo. Alimuomba Mwenyezi Mungu amsaidie katika hilo, na akasema kwamba changamoto haikuwa tu kuhifadhi Quran, bali pia kufuata maadili yake, kwani mwanadamu anapaswa kuwa mstari wa mbele katika maadili.

Abdel Jalil alisema kuwa alifuzu kwa mashindano haya ya kimataifa baada ya kushika nafasi ya kwanza katika Mashindano ya Kimataifa ya Port Said ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Misri mwaka 2019.

3485993

captcha