IQNA

Mafunzo ya Qur'ani

Zaidi ya wasichana na wavulana 22,000, washiriki katika Mashindano ya Qur'ani ya Qatar

12:52 - November 15, 2023
Habari ID: 3477893
DOHA (IQNA) – Toleo la 60 la Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu Qatar kwa wanafunzi wa shule yanaendelea katika nchi hiyo ya Kiarabu. Zaidi ya wavulana na wasichana 22,000 wanashiriki katika toleo hili la tukio la Qur'ani.

Wanawakilisha shule 533 zinazosimamiwa na serikali na zisizo za kiserikali nchini, kulingana na gazeti la Al-Ray. Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu ya Qatar imeandaa mashindano hayo kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu.

Jassim Abdullah al-Ali, afisa wa Wizara ya Wakfu, misikiti katika miji minne huandaa mashindano katika sehemu ya wavulana. Ameongeza kuwa kitengo cha wasichana kinafanyika katika vituo 9 vya Qur'ani katika miji tofauti. Wizara ya Wakfu ya Qatar imeweka uandaaji wa shughuli za Qur'ani Tukufu juu katika ajenda yake. Hivi karibuni ilifanya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaliyopewa jina la "bora zaidi".
Pia hupanga programu mbalimbali za elimu zinazohusisha ufundishaji wa Qur'ani Tukufu.
 
4181720

Kishikizo: qatar qurani tukufu
captcha