IQNA

Zifahamu Dhambi/9

Vigezo vya kutofautisha dhambi kuu na dhambi ndogo

14:20 - November 26, 2023
Habari ID: 3477952
TEHRAN (IQNA) – Kumekuwa na mijadala mingi miongoni mwa wanachuoni wa Kiislamu kuhusu ni vigezo gani vilivyopo vya kutaja dhambi kuwa kubwa (Kabira) au dhambi ndogo (Saghira).

Vigezo vitano vinavyotolewa na wanachuoni kwa madhambi makubwa ni kama vifuatavyo:

1- Dhambi yoyote ambayo Mwenyezi Mungu katika Qur'ani Tukufu ameahidi adhabu juu yake.

2- Dhambi yoyote ambayo Uislamu umeichukulia kuwa ni Hadd, kama vile kunywa mvinyo, zinaa n.k.

3- Dhambi yoyote inayoonyesha kudharau dini.

4- Dhambi yoyote iliyothibitishwa kwa dalili wazi kuwa ni Haramu na kubwa.

5- Dhambi yoyote ambayo Qur'ani na Sunnah imewaonya vikali wanaoifanya.

Kuhusu idadi ya madhambi makubwa, kumetajwa idadi tofauti, ikiwa ni pamoja na 7, 10, 20, 34 na 40.

Kwa mujibu wa kitabu,  Tahrir al-Wasilah  cha Imam Khomeini (RA), madhambi makubwa ni mengi, nayo ni pamoja na:

1- Kupoteza matumaini katika rehema za Mwenyezi Mungu

2- Kujisikia umesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu

3- Kunasibisha maneno yasiyo ya kweli kwa Mwenyezi Mungu, Mtume (SAW) na Maasumin (AS)

4- Mauaji

5- Kutowaheshimu wazazi

6- Kula mali za mayatima

7- Kukashifu wanawake wasio na dhambi

8- Kutoroka vitani

9- Kukata mahusiano ya kifamilia

10- Uchawi

11- Uasherati

12- Maingiliano ya jinsia moja

13- Wizi

14- Kuapa kwa uwongo

15- Kuficha ushuhuda

16- Kutoa ushahidi wa uongo

17- Kuvunja ahadi

18- Kutenda kinyume na mapenzi ya mtu

19- Kunywa mvinyo

20- Riba

21- Kula mali iliyopatikana kwa njia za Haramu

22- Kamari

23- Kula maiti za wanyama na kunywa damu

24- Kula nyama ya nguruwe

25- Kula nyama ya mnyama ambaye hajachinjwa kwa mujibu wa sheria ya dini

26- Kupunguza mizani wakati wa kuuza bidhaa

27- Kuhama kwenda mahali ambapo mtu atapoteza dini yake

28- Kuwasaidia madhalimu

29- Kuwategemea madhalimu

30- Kujiwekea haki za wengine

31- Uongo

32- Kiburi

33- Ufujaji

34- Upotovu

35- Kusengenya

36- Kupelekeza mambo ya wengine

37- Kujishughulisha na tafrija na pumbao nyingi

38- Kupuuza Hijja

39- Kuacha Salah

40- Kutotoa Zaka

41- Kusisitiza kufanya madhambi madogo.

Na bila shaka Shirki (ushirikina), kukataa aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, na uadui na watu wa Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa madhambi makubwa.

Kishikizo: dhambi
captcha