Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika siku ya Alhamisi katikati mwa jiji la Iran huku umati wa maafisa na wanazuoni wa kidini wakihudhuria.
Msahafu huo uimeandikwa na wanakaligrafia 26 wa kike huku mchakato huo ukichukua mwaka mmoja.
Mpango huo uliandaliwa na Darolketabeh ambayo ina uhusiano na Kituo cha Iran cha Uchapishaji na Usambazaji wa Qur'ani Tukufu.
Mkuu wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom, Ayatullah Seyyed Hashem Hoseini Bushehri, alikuwa mmoja wa wazungumzaji waliobainisha kuwa kuandika Qur'ani na kusoma aya kunapaswa kufuatwa kwa kutekeleza miongozo yake.
"Kusoma na kutazama aya huleta thawabu kwa hakika lakini, thawabu kuu huja tunapoelewa dhana na kutekeleza kile inachosema," aliongeza mwanazuoni huyo.
Mwishoni mwa sherehe, wanakaligrafia walikabidhiwa zawadi kwa mchango wao katika mradi huo.
4193389