IQNA

Uislamu

Vijana wa Madagaska Waandika Aya za Qur'ani Tukufu katika Ibada ya Itikaf

11:03 - February 01, 2024
Habari ID: 3478282
IQNA - Makumi ya vijana wa Kiislamu nchini Madagaska (Madagascar) walishiriki katika tukio la kipekee kama sehemu ya ibada ya Itikaf, iliyomalizika Januari 26, 2024.

Waliandika kwa mkono sura mbili za Qur'ani Tukufu , Surah Ad-Dhuha na Al-Inshirah, kwa maandishi ya Kiarabu.

Mkuu wa Kituo cha Imam Ridha (AS) katika mji mkuu Antananarivo, ambako ibada ya Itikaf ilifanyika, alipongeza kazi hizo hasa kwa kuzingatia kuwa vijana hao hawazungumzi Kiarabu.

Maandishi tisa bora zaidi yalitunukiwa zawadi.

Itikafu ni tukio la kiroho katika Uislamu ambalo linahusisha kukaa msikitini, kufunga, na kumwomba Mungu kwa idadi fulani ya siku.

Itikafu ni Sunna ya Mtume Muhammad (SAW) na familia yake, na inachukuliwa kuwa ni ibada yenye thawabu nyingi. Kwa kawaida hufanyika tarehe 13, 14, na 15 Rajab, mwezi wa saba wa kalenda ya Kiislamu.

Madagaska ni taifa la visiwa kusini mwa bara Afrika katika Bahari ya Hindi, ambapo Uislamu umekuwepo kwa karne nyingi. Takriban asilimia kumi ya wakazi wake ni Waislamu.

 

 

3487023

captcha