Maonyesho hayo ya Qur'ani Tukufu yalifunguliwa katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa kadhaa wa Iran na Thailand akiwemo Balozi wa Iran nchini Thailand Seyyed Reza Nobakhti, mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Thailand Mehdi Zare, na Naibu wa Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani Tukufu Alireza Moaf.
Mwanzoni mwa hafla hiyo, Mohammad Mehdi Azizzadeh, afisa wa Wizara ya Utamaduni ya Iran alitoa maelezo mafupi ya kazi za sanaa, bidhaa za Qur'ani na vitabu katika maonyesho hayo.
Akihutubia pia hafla hiyo, Phonpoom Vipattipumiprates, Naibu Waziri wa Utamaduni wa Thailand, alisifu utamaduni "tajiri" wa Iran, akibainisha kuwa nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano mkubwa wa kiutamaduni tangu kuanza kwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1955.
Hafla hiyo inayoangazia sanaa ya kisasa ya Qur'ani ya Iran, itasaidia kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiutamaduni na Kiislamu kati ya mataifa hayo mawili, alisema.
Moaf pia alihutubia tukio hilo, akibainisha kuwa maonyesho hayo yanaweza kupanuliwa kwa njia nyinginezo ikiwa Thailand iko tayari.
Maonyesho hayo yatakamilika Februari 11, 2024.
4198356