IQNA

Qur'ani Tukufu

Wizara ya Wakfu ya Kuwait yaandaa Mashindano ya Qur'ani ya Familia

14:51 - March 24, 2024
Habari ID: 3478567
IQNA - Toleo la 4 la Mashindano ya Familia ya Qur'ani lilianza nchini Kuwait siku ya Ijumaa.

Mashindano hayo yameandaliwa na Idara ya Misikiti ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu kwa kauli mbiu ya "Quran Inatuleta Pamoja", gazeti a Al-Ray limeripoti.

Jumla ya familia 143 kutoka kote Kuwait zinashiriki katika mashindano hayo ambayo hujumuisha usomaji na kuhifadhi Qur'ani miongoni mwa wanafamilia.

Watu watatu wa kila familia wanashiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani, akiwemo angalau mmoja wa wazazi.

Kulingana na Yusuf al-Sameiei, afisa wa kamati ya maandalizi, mashindano hayo yanalenga kukuza upendo wa Kitabu Kitakatifu miongoni mwa familia.

Alisema muda mwingi wa watoto leo unatumika katika mitandao ya kijamii na ni mapenzi ya Qur’ani ambayo huwakusanya wanafamilia.

Mashindano hayo yanafanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuleta familia za Kuwait pamoja, aliongeza.

/3487700

captcha