IQNA

Maadhimisho

Maadhimisho ya Miaka 21 ya Kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA)

10:57 - March 28, 2024
Habari ID: 3478593
IQNA- Makumi ya maafisa na wanaharakati wa Qur'ani wameadhimisha mwaka wa 21 wa kuanzishwa kwa kwa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA).

Sherehe za kuadhimisha tukio hilo zilifanyika Jumatano usiku katika banda la IQNA katika Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran.

Abbas Salimi, qari mkongwe wa Iran na mwanaharakati wa Qur'ani, alikuwa miongoni mwa wazungumzaji walioisifu IQNA kama "chimbuko la heshima" kwa jumuiya ya Qur'ani ya Iran.

Amehimiza uungwaji mkono zaidi kwa IQNA ili shirika hilo la habari liweze kusambaza ujumbe wa Qur'ani kote duniani.

Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA) ndilo shirika la kwanza na la pekee maalumu la habari za Qur'ani duniani.

Shirika hili Ilizinduliwa tarehe 15 Ramadhani, 1424, (Novemba 11, 2003) wakati wa sherehe iliyohudhuriwa na rais wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hivi sasa, Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani kila siku huchapisha habari na ripoti katika lugha 22 zikiwemo Kifarsi auKiajemi, Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kiurdu, Kiitaliano, Kichina, Kirusi, Kihispania, Kibengali, Kihausa, Kipashtu, Kihindi, Kituruki, Kiswahili, Kiazeri, Kifilipino, Kiindonesia, Kijerumani, Kimalei, Kireno na Kitajiki.

4207408

captcha