IQNA

Msikiti wa Al Aqsa

Wapalestina 125,000 wahudhuria Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa, wakaidi Israel

17:54 - March 30, 2024
Habari ID: 3478604
IQNA - Takriban waumini 125,000 wa Kipalestina walikusanyika katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa al-Quds (Jerusalem) kwa ajili ya sala ya tatu ya Ijumaa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani licha ya kuwekewa vikwazo vikali na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Azzam al-Khatib, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Wakfu za Kiislamu huko al-Quds, alibainisha kwamba idadi hii ya mahudhurio ilikuwa chini kuliko kawaida katika wakati huu wa Ramadhani. Mwaka jana, takriban waabudu 250,000 walikuwa wameshiriki sala siku kama  hiyo.

Mji wa al-Quds unaokaliwa kwa mabavu ulishuhudia wanajeshi wengi wa Israel wakitumwa kwa nguvu katika sehemu mbalimbali zikiwemo za kuingia. Zaidi ya hayo, milango ya nje ya Msikiti wa Al-Aqsa ilifuatiliwa kwa karibu, Shirika la Anadolu liliripoti.

Ruhusa za kuingia zilitolewa na mamlaka za Israel kwa wanaume walio na umri wa zaidi ya miaka 55 na wanawake walio na zaidi ya 50 ambao walitaka kuingia Quds Mashariki.

Wakati wa khutba yake ya Ijumaa, Sheikh Yusuf Abu Sneineh, mhubiri wa Msikiti wa Al-Aqsa, alikosoa jumuiya ya kimataifa kutochukua hatua kuhusiana na vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Isarel huko Gaza. Kampeni za kijeshi zinazoendelea zimewaacha Wapalestina wakikabiliwa na njaa kali kwa karibu miezi sita.

Zaidi ya Wapalestina wasiopungua 32,600, haswa wanawake na watoto, wameuawa na mashambulio ya Israeli huko Gaza tangu mapema Oktoba kwani mashambulio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa na kuyahama makaazi yao.

Katika uamuzi wa muda uliotolewa mwezi Januari, Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iliiamuru Tel Aviv kusitisha vitendo vya mauaji ya halaiki na kuhakikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia wa Gaza. Amri ya hivi majuzi ya mahakama inasisitiza haja ya dharura ya upatikanaji wa huduma za kimsingi bila vikwazo, ikiwa ni pamoja na chakula, maji, mafuta na vifaa vya matibabu.­­

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al aqsa sala ya ijumaa
captcha