IQNA

Nasaha

Rais wa Iran: Qur’ani Tukufu ina majibu kwa maswali yote ya maisha ya kisasa ya mwanadamu

18:32 - April 01, 2024
Habari ID: 3478614
IQNA - Rais wa Iran Ebrahim Raisi amesema Qur'ani Tukufu inaweza kujibu maswali yote ambayo wanadamu wanayo, akibainisha kuwa majibu haya yanaweza kupatikana kwa njia ya ijtihad.

"Qur’ani ina majibu ya maswali yote ya maisha ya kisasa ya mwanadamu. Leo, ni lazima tujitahidi kupata majibu haya kupitia ijtihad ya kujenga ustaarabu, tukiongozwa na nuru ya Quran Tukufu na aya zake tukufu,” Raisi alisema Jumamosi.

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika hafla ya kuwaenzi watumishi 15 wa Qur'ani wa Iran. Hafla hiyo ilifanyika kando ya Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran.

"Ingawa tumewaenzi watumishi wachache wa Qur'ani Tukufu leo, ni muhimu kutambua kwamba kila mtu anayehusika katika kuitumikia Qur'ani anastahili kuthaminiwa," alisema na kuongeza kuwa wamejitolea maisha yao kusoma, kuelewa na kuishi kwa kufuata aya za Mwenyezi Mungu katika Qur’ani.”

Mbinu za ubunifu katika Maonyesho ya Qur’ani

Raisi alitoa shukurani zake kwa waandaaji wote kwa kufanikisha maonyesho ya Qur'ani, sio tu mjini Tehran bali katika mikoa mbalimbali ya Iran mwaka huu. Pia alishukuru taasisi zote za Qur'ani, wanaharakati, na wanazuoni, hasa wale ambao wamechangia kazi mpya na zenye thamani kwa watoto na vijana katika maonyesho ya Qur'ani.

"Mwaka huu, tumeona muunganisho mzuri wa teknolojia na ubunifu katika maonyesho haya, ambayo ni mfano bora wa mbinu bunifu za elimu ya Qur'ani," alisema, akiashiria sehemu za ubunifu katika hafla hiyo zinazotumia teknolojia za kisasa kama vile akili mnemba (Artificial Intelligence) ili kukuza Qur’ an Tukufu.”

Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalizinduliwa rasmi katika sherehe za tarehe 20 Machi. Yamehudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 25.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu wa Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Huonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

Quran ni kimbilio la wote

Kwingineko, Rais Raeisi alisema kwamba Qur'ani Tukufu ni "kimbilio" la watu wote duniani kote. "Tunaamini kwamba ustawi na furaha ya mwanadamu inategemea kufuata aya za Qur'ani Tukufu, ambayo tunaiona kama kimbilio pekee la watu wote ulimwenguni."

Ufunguo wa kupata furaha katika maisha haya na akhera upo katika kuzingatia Quran, aliongeza.

Quran ufunguo wa umoja wa Waislamu

Kuzingatia Qur’ani kunasaidia kudumisha umoja wa Waislamu, alisisitiza. "Leo, siri ya umoja wa Waislamu na upinzani dhidi ya maadui iko katika kuzingatia Quran."

"Harakati za upinzani zenye nguvu tunazoziona leo ni ushahidi wa vilele vya utendaji vya Qur'ani Tukufu," alisema, na kuongeza kwamba uthabiti wa watu wanaodhulumiwa wa Gaza unatokana na kushikamana kwao na aya za Mwenyezi Mungu za Qur'ani Tukufu.

Quran inadhamini haki za binadamu, na cha kushangaza, wale wanaodai kwa uwongo kutetea haki za binadamu ndio wakiukaji wakubwa, Raisi alisema.

“Leo, pamoja na juhudi za wenye kiburi kutaka kupinga Qur’anI, hawatafanikiwa. Mapenzi ya Qur'ani Tukufu yanaongezeka katika nchi za Magharibi, na duniani kote, uzingatiaji wa Qur'an na Ahlul-Bayt (AS) unaongezeka," alisema.

3487753

Habari zinazohusiana
captcha