IQNA

Polisi wamuua Mwislamu Myanmar

16:56 - May 03, 2014
Habari ID: 1402630
Mwislamu aliyekuwa na umri wa miaka 65 amepoteza maisha baada ya kushambuliwa na polisi wa utawala wa Mabuddha nchini Myanmar.

Kwa mujibu wa ripoti wa mwandishi wa IQNA, Liyaqat Ali ameuawa katika mji wa Buli Bazar kaskazini mwa Mungado wakati alipokuwa akijaribu kumlinda kijana Mwislamu wa kabila la Rohingya aliyekuwa akitandikwa na polisi.
Kwingineko Wanaharakati wa haki za binadamu na makundi ya tiba ya kimataifa yametahadharisha kuhusu kuzidi kuzorota hali ya kiafya ya Waislamu wa kabila la Rohingya wa huko Myanmar. Taarifa za vyombo vya habari kila siku zinaripoti kuzorota kwa hali ya kiafya miongoni mwa Waislamu wa nchini Myanmar, huku wengi wakiishi katika mazingira ya kubaguliwa katika kitongoji cha Sittwe, makao makuu ya mkoa wa Rakhine.
Taarifa zinasema kuwa, wahanga wengi ni wanawake wajawazito na kwamba wale wanaoweza kustahmili hali hiyo, wanaachwa bila ya msaada, khususan baada ya wafanyakazi wa misaada wa kigeni kuamuriwa kuondoka nchini humo mwezi Februari mwaka huu. Hadi kufikia sasa ni Shirika la Chakula na Kilimo FAO pekee ndilo limeanza kugawa chakula kwa Waislamu wa Rohingya. Ripoti zinasema kuwa mamia ya maelfu ya Waislamu hao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na maji ya kunywa.
1402444

Kishikizo: myanmar waislamu
captcha