IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun

Msomi Maarufu cha Qur’ani Tukufu eneo la Balkan aaga dunia

19:19 - August 04, 2023
Habari ID: 3477380
BELGRADE (IQNA) – Sheikh Bayram Ayati, mtaalamu mashuhuri wa Qur’ani Tukufu katika nchi za Balkan amefariki dunia siku ya Jumatano.

Msomi huyo wa  Qur’ani  kutoka Seribia alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Ayati alikuwa mhadhiri  wa kitivo cha Chuo cha Mafunzo ya Kiislamu huko Novi Pazar, kusini magharibi mwa Serbia.

Aliwafunza wahifadhi wengi wa Qur’ani Tukufu kwa miaka mingi.

Sheikh Bayram alikuwa mtoto wa marehemu Sheikh Afiq Ayati, anayejulikana kama mmoja wa walimu bora wa Qur'ani katika Balkan.

Kulingana na sensa ya 2022, kulikuwa na Waislamu wapatao 280,000 nchini Serbia, na hivyo kuwa asilimia 4.2 ya jumla ya wakazi.

Mkusanyiko mkubwa zaidi wa Waislamu nchini Serbia unaweza kupatikana katika manispaa za Novi Pazar, Tutin, Sjenica na Prijepolje katika eneo la Sandžak, na katika manispaa ya Preševo na Bujanovac katika Bonde la Preševo.

Eneo la Balkan linajumuisha Albania, Bosnia-Herzegovina, Bulgaria, Kosovo, Montenegro, Makedonia, Serbia.

4159903

Kishikizo: serbia balkan waislamu
captcha