IQNA

Uislamu nchini Ghana

Waislamu Ghana wazindua Baraza lao la umoja na maendeleo

21:15 - December 14, 2022
Habari ID: 3476250
TEHRAN (IQNA) – Baraza la Umoja na Maendeleo ya Waislamu limezinduliwa nchini Ghana kwa lengo la kukuza mshikamano na ustawi wa jamii ya Waislamu katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Baraza la Waislamu la Mkoa wa Kaskazini lenye wanachama 29, ambalo litatumika kama mwavuli wa umoja na maendeleo kwa madhehebu yote ya Kiislamu nchini Ghana lilizinduliwa mwishoni mwa juma huko Tamale, mji mkuu wa Mkoa wa Kaskazini.

Baraza hilo linaundwa na wajumbe wenye utaalamu wa fani mbalimbali kama vile utabibu, dini, uhasibu, na utawala ili pamoja na mengine kusaidia kukuza umoja kati ya Waislamu na taifa kwa ujumla.

Naye Waziri wa Kanda ya Kaskazini Alhaji Saani Alhassan Sayibu kwa niaba ya Makamu wa Rais na Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi huo Dk Mahamadu Bawumia amewataka wajumbe wa baraza hilo kuwa waaminifu na wawe na uwazi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Pia aliwapa jukumu la kufanya kazi na madhehebu zote ya Kiislamu ndani ya eneo na mashirika mengine ya kidini ili kukuza umoja na maendeleo katika utofauti.

Mwenyekiti wa Baraza na Meneja wa Mkoa wa Kitengo cha Elimu ya Kiislamu, Issah Alhassan Abubakari, akitoa maelezo yake alisema baraza hilo litakuwa chombo mwamvuli wa Madhehebu ya Waislamu wot wa Mkoa wa Kaskazini.

Pia alisema baraza hilo litasaidia kukuza ufahamu bora wa Uislamu kupitia mafundisho na ujifunzaji wa misingi na mafundisho ya Kiislamu yaliyopo katika Qur'an na Sunnah, kuchukua hatua za kivitendo za kuhimiza na kuhakikisha Waislamu wanaishi kwa kufuata mafundisho ya Uislamu na kuendeleza umoja, upendo, amani, nia njema na maelewano miongoni mwa madhehebu za Kiislamu kwa njia ya mazungumzo endelevu.

3481676

Kishikizo: ghana waislamu
captcha