IQNA

CAIR: FBI iache ujasusi misikitini nchini Marekani

20:33 - November 15, 2014
Habari ID: 1473495
Kiongozi mwandamizi wa Baraza la Uhusiano wa Kiislamu nchini Marekani (CAIR) ameitaka Polisi ya Marekani FBI kuacha kufanya ujasusi ndani ya Misikiti nchini humo.

Akizungumza kwa niaba ya Waislamu, Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR huko Minnesota Lori Saroya amesema kuwa, wafanyakazi wa FBI wamekuwa na tabia ya kutembelea na kuingia misikitini katika miji ya Saint Paul, Minneapolis na miji mingine katika jimbo la Minnesota, kwa lengo la kuwarubuni baadhi ya Waislamu ili wafanye ujasusi dhidi ya Waislamu wenzao. Saroya amesisitiza kwamba wafuasi wa dini ya Kiislamu wanaelewa majukumu yao ya kidini na kijamii ya kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola, pindi wapoona dalili za kufanyika uhalifu na jinai. Amesisitiza kwamba polisi wa FBI wanapoingia kwenye maeneo ya ibada hasa misikitini, husababisha hali ya hofu na wasiwasi kwa waumini wa dini hiyo. Amesema kuwa, kitendo cha kuwarubuni Waislamu ili wafanye ujasusi dhidi ya Waislamu wenzao kinakinzana na misingi ya kidini na kiakhlaki.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, msemaji wa FBI amekataa kutoa tamko kuhusiana na tuhuma hizo zilizotolewa dhidi ya Polisi ya Marekani.

1471835

captcha