IQNA

Sayyid Nasrallah awapongeza wapigania ukombozi Palestina

21:20 - October 18, 2015
Habari ID: 3388690
Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Lebanon ya Hizbullah amewapongeza wanaharakati wanaopigania ukombozi wa Palestina kwa kujitolea muhanga na kusimama kidete katika Intifadha ya 3 inayoendelea hivi sasa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Tukufu.

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo hii leo wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Hassan al-Haji, mmoja wa waliokuwa makamanda waandamizi wa Hizbullah aliyeuawa na matakfiri wa ISIS au Daesh nchini Syria.

Sayyid Nasrallah amesema maadui hawawezi kujihisi salama maadamu mapambano yanaendelea na kwamba Intifadha ndiyo njia pekee ya kuutokomeza utawala wa Kizayuni wa Israel unaozikalia ardhi za Palestina kimabavu. Katibu Mkuu wa Hizbullah amekariri kuwa wanaunga mkono kikamilifu Intifadha ya taifa la Palestina na kwamba kinachoshuhudiwa hivi sasa huko Quds (Jerusalem), Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Ukanda wa Ghaza na katika maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni tangu 1948, ni Intifadha ya 3 ya kuilinda mji wa Quds..

3387225

captcha