IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

Hizbullah: Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni dalili ya ujasiri wa Wapalestina

21:54 - November 08, 2023
Habari ID: 3477859
BEIRUT (IQNA) - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Hizbullah ya Lebanon amesema Operesheni ya Kimbunge cha al-Aqsa kama kielelezo cha ujasiri, na uchamungu waa watu wa Palestina.

Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa dhidi ya utawala wa Israel "ni operesheni ya kipekee ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu kuasisiwa utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 1948 na tunaamini itakuwa hatua ya mabadiliko kwa siku zijazo," Sheikh Naim Qassem alisema wakati wa mahojiano. na kipindi cha “Ana kwa Ana” cha Press TV siku ya Jumanne.

"Operesheni hii ilipanda mbegu ambayo inaweza kusababisha kurudi nyuma na kuanguka kwa utawala, wa Israsen kwani iliweza kubaini kuwa uwezo wa usalama wa Israeli ni dhaifu sana. Jeshi la Israel ni dhaifu sana. Na wanasiasa hawajui lolote na hawawezi kufikiria siku zijazo,” aliongeza.

Sheikh Qassem aliendelea kusema kuwa Israel ni "utawala bandia" ambao hauna  nguvu."

Afisa huyo wa Hizbullah aliendelea kubainisha kwamba "Operesheni kubwa na ya ajabu" ya Kimbunga cha al-Aqsa ilikuwa kazi wanamapambano wa Kiislamu wenye heshima na ushawishi mkubwa" na "ilikuwa ni dalili ya ujasiri na uchamungu " wa Wapalestina.

Sheikh Qassem pia alibainisha kuwa lengo la makundi yote ya muqawama ni kuishinda Israel na kupata ushindi. Kwa hivyo, alisema, vikundi vya muqawama vinahitaji kushirikiana kwani "operesheni hii ilikuwa na mafanikio makubwa."

Kuhusiana na hatua ya kijeshi ya Hizbullah ya kuwaunga mkono Wapalestina, Sheikh Qassem amesema ushiriki wa Harakati ya Hizbulla katika vita vya Gaza ni sehemu ya operesheni ya wanamapambano wa Palestina na kusisitiza kuwa, juhudi za pamoja zinahitajika ili kukomesha hujuma ya Israel dhidi ya raia wa Gaza.

Hizbullah imekuwa ikihusika katika mapigano na Israel ilipoanzisha uvamizi wa kila upande huko Gaza mwezi uliopita.

Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayed Hassan Nasrallah alisema siku ya Ijumaa kuwa chaguzi zote ziko mezani dhidi ya Israel na kuutaka utawala wa Kizayuni uache mara moja hujuma dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

Hayo yanajiri wakati ambao, Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa idadi ya waliouawa shahidi kutokana na mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo imeongezeka na kufikia 10,569.

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza leo (Jumatano, tarehe 8 Novemba) ikiwa ni siku ya 33 ya operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa" takwimu za karibuni kabisa za wahanga wa mashambulizi mtawalia ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa ripoti hii, idadi ya mashahidi wa vita vya Gaza katika siku ya 33 ya mashambulizi ya utawala huo ghasibu imefikia watu 10,569, kati yao 4,324 ni watoto na 2,823 ni wanawake.

Ashraf al-Qadra, msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza, ametangaza kwamba kesi  2550 zimesajiliwa  huko Gaza hadi sasa za watu waliopotea, ambapo 1,350 ni watoto na bado wako chini ya vifusi.

Habari zinazohusiana
captcha