IQNA

Wasomaji Qur’ani wa Mauritania watembelea Karbala, Iraq

22:35 - November 17, 2021
Habari ID: 3474571
TEHRAN (IQNA) Kundi la wasomaji na wanaohifadhi Qur’ani Mauritania wametembelea Haram Takatifu ya Imam Hussein AS mjini Karbala, Iraq.

Ujumbe huo wa Mauritani, ambao umefika Karbala kufuatia mwaliko wa Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS, pia umejumuisha pia maimamu wa misikiti katika nchi hiyo ya  Afrika.

Wageni hao wametembelea idhaa ya Qur’ani na kusikiliza kipindi kilichokuwa kinarushwa hewani na qarii mashuhuri wa Iraq Ustadh Ali Al Khafaji. Ujumbe huo pia umejadili kuhusu ushirikiano katika uga wa Qur’ani na Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyo katika eneo Maghreb, kaskazini magharibi mwa Afrika. Idadi ya watu nchini humo ni milioni nne na karibu Wamauritani wote ni Waislamu. Nchi hiyo ni maarufu kwa harakati zake za Qur’ani.

میزبانی آستان مقدس حسینی از گروه قرآنی موریتانی + عکس

میزبانی آستان مقدس حسینی از گروه قرآنی موریتانی + عکس

4013796

captcha