IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu kwa sauti ya Wamauritani kurekodiwa

19:37 - August 07, 2021
Habari ID: 3474169
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Vijana, Michezo nchini Mauritania ametangaza kufunguliwa vituo vya kurekodi na kusambaza qiraa ya Qur'ani Tukufu kwa sauti ya wasomaji wa Mauritania.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la  Mauritania, Seyed Mohammad Ould Aswaidat, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Vijana, Michezo na Maingiliano na Bunge la Mauritania, alisema: Kazi ya kurekodi imeanza Ijumaa Agosti 6  ambapo qiraa kamili ya Qur'ani Tukufu itarekodiwa kwa wasomaji wa Mauritani na kazi hiyo itamalizika baada ya mwezi."

Waziri huyo amesifu juhudi za Redio Mauritania kutokana na jitihada zake katika kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu na Sunna ya Mtume SAW.

Naye Seyed Mohammad Mukhtar Ould  Anbalal, mwenyekiti wa Baraza la Kielimu katika Redio ya Mauritania, pia amesisitiza umuhimu wa kufanya mikutano ya Qur'ani na Sunnah, huku akitoa wito kwa Waislamu  kuendelea kusoma Qur'ani ndani majumbani na misikitini.

3988854

captcha