IQNA

Waislamu Mauritania

Nakala 300,000 za Qur'an Tukufu zasambazwa nchini Mauritania

17:32 - September 29, 2023
Habari ID: 3477667
NOUAKCHOTT (IQNA) - Mauritania imeanza kusambaza nakala 300,000 za Qur'ani Tukufu katika misikiti ya nchi hiyo.

Waziri wa Awqaf (Wakfu) na masuala ya Kiislamu alitangaza hili, akibainisha kwamba Misahafu hiyo ni ya muundo wa Warsh na Qaloun kutoka katika riwaya ya Nafi.

Alisema Misahafu 100,000 itasambazwa katika misikiti ya mji mkuu Nouakchott na iliyosalia katika majimbo mengine.

Waziri huyo alibaini kuwa baadhi ya Misahafu iliyokuwa na makosa ya chapa tayari imekusanywa kutoka misikitini kwa amri ya rais wa Mauritania.

Kamati ya Qur'ani Tukufu ya Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu imesimamia uchapishaji na usambazaji wa Misahafu hiyo mipya, alisema.

Misahafu iliyoandikwa kwa mtindo wa qiraa ya Warsh na Qaloun kwa mujibu wa riwaya ya Nafi ni mashuhuri  katika nchi za Afrika Kaskazini na Magharibi, mbali na Misri.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb magharibi mwa Afrika Kaskazini. Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa takriban milioni 4 na takriban Wamauritania wote ni Waislamu. Shughuli na programu za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi ya Kiafrika.

.

300,000 Copies of Quran Being Distributed in Mauritania

 300,000 Copies of Quran Being Distributed in Mauritania

4171547

captcha