IQNA

Mgogoro wa kisiasa Iraq

Iran yawapongeza Wairaqi kwa kutumia hekima kukabiliana na fitina

15:29 - August 31, 2022
Habari ID: 3475708
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ilitoa tamko kuhusiana na matukio ya hivi majuzi nchini Iraq na kusisitiza kuwa: "Tehran daima inataka Iraq yenye utulivu, salama na yenye nguvu."

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran inasema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza kuridhishwa kwake na kurejeshwa amani nchini Iraq na inawaombea maghfira waliopoteza maisha na kuwatakia afya njema waliojeruhiwa katika matukio ya hivi karibuni."

Halikadhalika Iran imewapongeza wananchi na serikali ya Iraq kwa kutumia hekima kukabiliana na fitina iliyosababisha ghasia na fujo nchini humo.

Iraq imekuwa ikishuhudia migogoro wa kisiasa kwa muda mrefu. Baada ya uchaguzi wa bunge wa Oktoba 2021, mzozo wa kuundwa kwa serikali ulianza, kisha Moqtada Sadr, kiongozi wa harakati ya Sadr ya Iraq, aliwataka wawakilishi 73 wa harakati hii kujiuzulu; Baada ya kujiuzulu wawakilishi wa Harakati ya Sadr, Kamati ya Uratibu ya Vyama vya Mashia wa Iraq, katika kikao na baadhi ya vyama vya Iraq, ilisisitiza juu ya kuharakisha mchakato wa kuunda serikali nchini Iraq.

Muqtada Sadr siku ya Jumatatu (Agosti 29) kwa kutangaza kujiondoa katika siasa, alisababisha duru nyingine ya mvutano nchini Iraq, ambayo hata ilisababisha migogoro ya umwagaji damu katika nchi hii. Kufuatia tangazo la kujiuzulu kwake katika ulimwengu wa siasa, wafuasi wa Sadr walishambulia ikulu ya rais, ikulu ya waziri mkuu na Baraza la Juu la Mahakama mjini Baghdad na kusababisha makumi ya watu kuuawa na mamia kujeruhiwa.

Maendeleo ya Iraq ni muhimu kwa Iran kwa njia nyingi; Miongoni mwa nchi za Kiarabu za eneo la Magharibi mwa Asia, Iraqi ina mafungamano makubwa zaidi ya kiutamaduni na kidini na Iran. Aidha mpaka wake na Iran una urefu wa karibu kilomita 1258 wa nchi kavu na kilomita 351 baharini, uhusiano kikaumu, kihistoria, kilugha, umoja wa kidini, na kuwepo kwa vitisho na usalama wa pamoja na maslahi ya kiuchumi ya pamoja ni kati ya nukta muhimu katika mahusiano ya Iran-Iraq. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukipanuka katika miaka ya hivi karibuni katika fremu ya sera za  ujirani mwema. Wakuu wa Baghdad na Tehran wamekuwa wakisisitiza kuhusu uimarishaji wa pande zote wa uhusiano.

Kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, suluhu pekee la kujiondoa Iraq katika mgogoro wa sasa ni kufuatilia njia zenye mwelekeo wa mazungumzo, kushikamana na katiba na michakato ya kisiasa. Iwapo makundi na mirengo ya kisiasa ya Iraq  itakubali uwajibikaji  na iwe na ushiriki amilifu katika mchakato wa kisiasa, basi hilo linaweza kuwa msingi sahihi wa kuundwa kwa serikali mpya na kumaliza mgogoro na migogoro ya sasa.

Katika taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran pia imeelezwa kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaitaka mirengo yote ya kisiasa, shakhsia na wale wanaopenda kuwa na Iraq yenye nguvu na uhuru, kuheshimu haki na matakwa ya kila mmoja wao katika mchakato wa amani na mazungumzo." Aidha Iran imeitaka mirengo ya kisiasa  Iraq kuwa na mwelekeo wenye uwajibikaji wa kisiasa na kijamii, kufuata matakwa na vitendo vyao vyote kwa kuzingatia sheria na njia za kisheria za nchi na  katika mazingira ya sasa kuziba njia kwa wale wote wenye nia mbaya dhidi ya Iraq.

3480294

captcha