IQNA

Shakhsia katika Qur'ani Tukufu /25

Mwokozi wa Bani Isra’il

19:07 - January 07, 2023
Habari ID: 3476367
TEHRAN (IQNA) – Bani Isra’il walikuwa kaumu kubwa katika historia. Walikuwa wamepewa dhamana ya kufika ardhi waliyoadhiwa na Mwenyezi Mungu ambaye alimpa Nabii Musa (AS) jukumu la kuwaokoa. Bani Isra’il waliokolewa lakini walibadili hatima yao kwa kutomtii Mwenyezi Mungu.

Nabii Musa (AS) alikuwa wa ukoo wa Lawi, mtoto wa Yakub (AS). Yeye ni Ulu al-Azm mjumbe wa tatu wa Mwenyezi Mungu baada ya Nuhu (AS) na Ibrahim (AS). Musa (AS) anajulikana kama Kalimullah (mtu anayezungumza na Mwenyezi Mungu). Alipewa cheo hicho kwa sababu alizungumza na Mungu moja kwa moja.

Wengi wa wafuasi wake walitoka kwa Bani Isra’il na wale wanaomfuata Musa (AS) wanaitwa Mayahudi. Maneno yote mawili, Bani Isra’il na Myahudi, yametajwa ndani ya Qur'ani Tukufu.

Jina la Musa limetajwa katika Qur'ani Tukufu mara 136 na katika visa 420, marejeo yanafanywa kwenye hadithi yake na matukio makubwa katika maisha yake. Jina lake limekuja katika Sura Al-Baqarah, Al Imran, An-Nisa, Al-Ma'idah, Al-An'am, Al-A'raf, Yunus, Hud, Ibrahim, Al-Isra, Kahf, Maryam, Al- Anbiya, Ash-Shua'ra, An-Naml, Al-Qasas, Al-Ahzab, Safat, Ash-Shura, Zukhruf, An-Nadhiat, na Al-A'ala.

Wakati mmoja, alipomwona mtu wa Misri akimshambulia mtu kutoka Bani Isra’il, Musa alimlinda mtu huyo aliyeonewa na kumpiga yule Mmisri kifuani. Mtu huyo alikufa na Musa akatoroka Misri.

Alikwenda Madyan, ambako alikutana na wasichana waliokuwa wakichunga kondoo. Musa (AS) aliwasaidia katika kuwanywesha kondoo na akafuatana nao hadi nyumbani kwao.

Hao walikuwa mabinti wa Shuaib (AS). Walimsihi baba yao kumwajiri Musa (AS) naye akakubali. Kisha Shuaib (AS) baada ya kumalizika kwa mkataba, Musa alioa mmoja wa binti za Shuaib.

Alipokuwa akirudi Misri, Musa (AS) aliona mwanga kutoka Mlima Tur (Sinai) na akauendea. Alipofika pale, alisikia sauti, ambayo ilikuwa ni sauti ya Mwenyezi Mungu ikizungumza na Musa (AS) na kumpa habari za kuteuliwa utume.

Alipewa jukumu la kwenda kwa Firauni na kumwalika kwenye Tauhidi. Firauni  alikataa mwaliko wake na akajaribu kuwaangamiza Musa na wafuasi wake.

Musa na Bani Isra’il walitoroka kutoka Misri na watu wakaokolewa kutoka kwa dhalimu na watu wake.

Bani Isra’il walisogea kuelekea nchi ya ahadi, ambayo inasemekana kuwa ni Sham na wakawa na nguvu kwenye njia. Walipaswa kwenda vitani lakini wakatoa visingizio na kumwambia Musa kwamba yeye na Mungu wake wanapaswa kupigana vita. Kwa sababu ya kutotii kwao, watu hao walihukumiwa kukwama katika jangwa kwa miaka 40 na kupigwa marufuku kuingia katika nchi ya ahadi. Katika kipindi hiki, walikumbana na matatizo kama vile njaa na kiu na matatizo hayo yaliondolewa kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Katika kipindi hicho, Musa (AS) alikufa akiwa na umri wa miaka 120 au 126. Kifo chake kinasemekana kuwa kilitokea katika karne ya 17 KK.

Kishikizo: musa bani israil
captcha