IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Mashindano ya kitamaduni yamepangwa kwa ajili ya Vituo vya Kuhifadhi Qur'ani vya Misri

15:24 - January 18, 2023
Habari ID: 3476423
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Wakfu ya Misri imezindua mipango ya kuandaa mashindano ya kitamaduni mtandaoni kwa wanafunzi wa vituo vya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini humo.

Mashindano hayo yatafanyika katika muhula wa pili wa mwaka wa shule wa 2022-2023, wizara ilisema.

Katika mashindano ya kila wiki, maswali hupewa wanafunzi kila Jumapili na wana hadi Jumatano kuwasilisha majibu yao mtandaoni.

Washindi watatangazwa wiki ijayo na vituo vitatu vya Qur'ani vyenye majibu sahihi zaidi pia vitachaguliwa kuwa vituo vya juu zaidi.

Washindi na wasimamizi wa vituo vya juu watapokea zawadi za pesa taslimu na cheti cha heshima, wizara ilisema.

Katika hatua nyingine, Wizara ya Awqaf ya Misri imesema itaandaa halka ya Qur'ani Tukufu katika Msikiti wa Imam Hussein (AS) katika mji mkuu Cairo kwa kushirikisha wasomaji au maqarii maarufu wa Qur'ani Tukufu..

Wasomaji wakuu wa Qur'ani watakaohudhuria programu hiyo ya Qur'ani Tukufu ni pamoja na Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina, Sheikh Mahmoud Muhammad al-Khisht, Sheikh Taha al-Numani, Sheikh Yasir al-Shraqawi, Sheikh Ahmed Iwaz Abu Fuyuz, Sheikh Ahmed Tamim al-Maraqi, na Sheikh YusufHalawa.

4114978

captcha