IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

ACECR: Kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kunaonyesha chuki dhidi ya Uislamu

16:17 - January 28, 2023
Habari ID: 3476479
TEHRAN (IQNA) - Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR) imelaani vikali vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu barani Ulaya, na kubainisha kwamba vitendo hivyo viovu vinaonyesha "chuki kubwa" ya maadui dhidi ya Uislamu.

Katika taarifa yake siku ya Jumamosi, ACECR ilikashifu vikali kudhalilishwa kwa Qur'ani Tukufu hivi karibuni katika nchi za Ulaya.

Akademia hiyo ya kimapinduzi ilianza taarifa yake kwa aya ya 8 ya Sura Ass'af “Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.."

Taarifa hiyo imesema: "Hatua za uovu za askari wa kijahilia katika kumdharau Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na Qur'ani Tukufu ni "ishara ya wazi ya kinyongo chao,." na kuongeza kuwa vitendo hivyo havina matokeo yoyote isipokuwa kukuza zaidi "utamaduni wa imani ya Mungu mmoja" ulimwenguni.

Mwenyezi Mungu ameahidi kuilinda Qur'an: " Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda." [Sura Al-Hijr, aya ya 9] na Mwenyezi Mungu atavinja njama za maadui “..Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu.” [Surah Ghafir, aya ya 25], imeongeza taarifa hiyo hiyo.

Wajibu wa kila Muislamu, imesema taarifa hiyo, ni kushikamana na Qur'an Tukufu "ambayo ni muongozo wenye nuru na kutekeleza mafundisho yake katika maisha binafsi na ya kijamii.

"Jibu kali zaidi kwa hatua hizi za upofu ni kupata ujuzi wa kutosha wa aya za Qur'ani na kutekeleza mafundisho yao ya uzima," ACECR iliongeza.

Kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu  kamwe hakuwezi kusimamisha njia inayong'aa ya ustaarabu wa Kiislamu, ilisema taarifa hiyo na kuongeza, "Kwa kawaida, vitendo vya kupinga dini na wendawazimu chini ya kivuli cha nara kama vile uhuru wa kujieleza vimefichua uso na mikono chafu ya madola ya kibeberu na uovu wao."

Akademia hiyo imewataka viongozi wa kidini, wapenda uhuru na wasomi wa ulimwengu wa imani ya Mungu mmoja kulaani uenezaji chuki wa hivi karibuni na kuweka mipaka ya wazi baina yao na wahusika wa vitendo hivyo viovu na pia waeleze mshikamano wao na ulimwengu wa Kiislamu ili kuzuia migawanyiko miongoni mwa Umma wa Ibrahim.

Jumamosi iliyopita Rasmus Paludan, mwanasiasa mwenye misimamo mikali wa Denmark alichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu karibu na Ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm huku akiwa analindwa na polisi ya Uswidi. 

Aidha siku ya Jumapili, Edwin Wagensveld, mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Uholanzi, na kiongozi wa kundi la chuki dhidi ya Uislamu la Pegida, alirarua kurasa za Qur’ani Tukufu huko The Hague, mji mkuu wa Uholanzi. Video ya Wagensveld kwenye Twitter ilionyesha kuwa alichoma kurasa zilizochanwa za Qur’ani Tukufu.

Vitendo hivi vinaendelea kulaaniwa vikali na Waislamu pamoja na nchi za Kiislamu duniani ambapo serikali za Sweden na Uholanzi zimekosolewa kwa kuunga mkono vitendo hivyo viovu.

4117698

captcha