IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Al-Azhar kujadili 'Uhalifu wa Kuchoma Qur'ani Tukufu katia nchi za Magharibi

16:57 - August 01, 2023
Habari ID: 3477366
CAIRO (IQNA) - Semina itaandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kujadili kukabiliana na uhalifu wa uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu katika nchi za Magharibi.

Ni sehemu ya semina za kila wiki za kituo hicho zinazofanyika katika Msikiti wa Al-Azhar mjini Cairo ili kutoa majibu ya maswali na shaka kuhusu masuala ya Kiislamu.
Semina hiyo itafanyika chini ya usimamizi wa mkuu wa Al-Azhar Sheikh Ahmed al-Tayyeb, ambapo wanazuoni na wasomi wa Misri Abdul Munim Fuad, Abdul Fattah al-Awari, Jamil Taaleeb na Majdi Abdulghaffar watakuwa miongoni mwa wazungumzaji wa hafla hiyo.
Abdul Munim Fuad, ambaye ni msimamizi mkuu wa shughuli za kitaaluma za Al-Azhar, alisema semina hizo za kila wiki zinalenga kuondoa mashaka na kujibu maswali kuhusu masuala tofauti ya dini.
Katika wiki za hivi karibuni, wimbi jipya la vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu vimeanza nchini Uswidi na Denmark.
Nchi hizi za eneo la Nordic barani Ulaya zinaruhusu kufuru hizo kutokea chini ya kivuli cha kile kinachoitwa uhuru wa kujieleza licha ya kulaumiwa vikali na mataifa ya Kiislamu na yasiyo ya Kiislamu na hata mbele ya azimio la Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mapema mwezi huu.

3484596

 

Habari zinazohusiana
captcha