IQNA

Shakhsia katika Qur'ani /53

Kwa nini Jina la Shetani Linarudiwa katika Qur'ani Tukufu?

19:10 - October 30, 2023
Habari ID: 3477814
TEHRAN (IQNA) – Tukiangazia aya za Qur’ani Tukufu tunaona kwamba shetani ana njia nyingi za kujipenyeza nyoyo za watu na kwamba bila ya kumwamini Mungu kwa nguvu, mtu hawezi kupinga vishawishi vya Shetani.

Baada ya Shetani kumwasi Mwenyezi Mungu na kukataa kumsujudia Adamu (AS), alifukuzwa kutoka peponi. Kisha akaahidi kujaribu kuwapotosha wanadamu wote. Hili limefafanuliwa katika Aya ya 50 ya Surah Al-Kahf:

“Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipo kuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu."

Tukio hili limetajwa katika aya zingine kadhaa za Qur'ani Tukufu ili kuweka msisitizo juu ya ukweli kwamba Shetani ni adui wa wanadamu bila shaka na lengo lake ni kuwapoteza. Kwa mujibu wa Aya ya 16-18 ya Surat Al-A’araf:

Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani.

Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Tangu mwanzo kabisa, Shetani alianza uadui wake mkali dhidi ya wanadamu kwa nguvu zake zote na chochote alicho nacho. Wahasiriwa wa kwanza walikuwa Adam (AS) na Hawa:

“Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele." Aya ya 20 ya Surah Al-A'raf)

Hii ilikuwa changamoto ya kwanza katika makabiliano ya mwanadamu na Shetani na kuanzia hapo na kuendelea, alikabiliana na aina mbalimbali za majaribu ya Shetani hivyo atajaribiwa katika majaribu ya kimungu kwa njia tofauti.

3485795

captcha