IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Viongozi wa Kiislamu Marekani wadai haki wakati wa Mazishi ya Imam aliyeuawa Newark

12:04 - January 07, 2024
Habari ID: 3478160
IQNA - Mamia ya waombolezaji walistahimili baridi siku ya Jumamosi kuhudhuria mazishi ya Imam Hassan Sharif, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatano alipokuwa akitoka kwenye swala ya asubuhi kwenye msikiti mmoja huko Newark.

Mazishi hayo, yaliyofanyika katika Msikiti wa Newark, yaliwavutia viongozi wa Kiislamu kutoka kote New Jersey, ambao walimsifu Sharif kama imamu aliyejitolea na mwenye huruma ambaye alitumikia jumuiya yake kwa miaka mitano huko Masjid Muhammad-Newark.

Pia walionyesha hasira kutokana na kukosekana kwa maendeleo katika uchunguzi wa mauaji yake, ambayo walisema ni sehemu ya mtindo mpana wa ghasia na chuki dhidi ya Waislamu nchini humo.

Mamlaka haijatambua mshukiwa au sababu zozote za ufyatuaji risasi huo, uliotokea nje ya Msikiti wa Majid Muhammad mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi siku ya Jumatano. Wamesema hakuna ushahidi kwamba Sharif, 46, alilengwa kwa sababu ya imani yake.

Lakini viongozi wa Kiislamu waliozungumza katika mkutano na wanahabari kabla ya mazishi walisema hawakuamini kwamba kifo cha Sharif kilikuwa kitendo cha kawaida cha uhalifu. Waliashiria kuongezeka kwa uhalifu wa chuki na unyanyasaji dhidi ya Waislamu tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, wakati utawala haramu wa Israel ulipanzisha vita dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

" Waislamu, kwa mara nyingine tena wametikiswa hadi kwenye msingi wao," alisema Dina Sayedahmed, msemaji wa tawi la  New Jersey ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani, au CAIR.

Sami Shaban, msemaji wa Muungano wa Waislamu wa New Jersey, alisema Sharif alikuwa "kito na ndugu kwa wengi wetu."

Imamu Daud Haqq, rais wa Baraza la Maimamu la Newark, alisema misikiti ilipaswa kuwa "maeneo ya usalama, kama maeneo yote ya kidini," lakini mauaji ya Sharif "yalikiuka moja kwa moja nafasi hiyo ya usalama na utakatifu."

3486709

Habari zinazohusiana
Kishikizo: marekani cair waislamu
captcha