IQNA

Matembezi ya Arbaeen

Rais wa Iran: Arbaeen ni dhihirisho la muqawama na mapambano ya Kiislamu

18:07 - September 17, 2022
Habari ID: 3475798
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja Arbaeen (Arubaini) ya Imam Hussein AS kuwa ni muujiza wa Mwenyezi Mungu na moja ya madhihirisho na vielelezo vya umoja wa Waislamu na akasisitiza kuwa: Ashura ingali hai na itaendelea kuwa hai.

Akiwa katika matembezi ya Arbaeen mjini Tehran, Sayyid Ebrahim Raisi ameongeza kuwa: "Arubaini ya Imam Hussein inaonyesha umoja na mshikamano wa Waislamu" na kuongeza kuwa: Arubaini pia ni dhihirisho la muqawama na mapambano ya Kiislamu na inaonyesha kwamba Ashuraa bado iko hai na itabakia hai.

Leo Jumamosi, tarehe 20 Safar 1444 Hijria (17 Septemba 2022), ni siku ya arubaini tangu baada ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad SAW na masahaba zake waaminifu katika jangwa la Karbala tarehe 10 Muharram mwaka 61.

Katika siku hii ya leo mamilioni ya Waislamu kutoka pande zote za dunia, ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wako katika mji mtakatifu wa Karbala ulioko kusini mwa Iraq kuhudhuria shughuli hiyo ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Aidha wale ambao hawakuweza kufika Karbala leo wameshiriki katika matembezi ya malaki katika miji yao ambapo mjini Tehran makumi ya maelfu ya waumini wamejitokeza kushiriki matembezi ya Arbaeen.

https://farsi.iranpress.com/iran-i219954

captcha