IQNA

Arbaeen 1445

Haram Takatifu za Karbala, Najaf zatangaza mipango ya kuwahudumia Wafanyaziara wa Arbaeen

18:05 - August 22, 2023
Habari ID: 3477481
BAGHDAD (IQNA) – Wasimamizi wa Haram Takatifu Imam Ali (AS) huko Najaf na Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala, Iraq wametangaza mipango ya kuwahudumia wanaozuru maeneo mawili matakatifu wakati wa msimu wa Arbaeen.

Haidar Rahim, afisa wa masuala ya vyombo vya habari Haram ya Imam Ali (AS) alisema programu hizo ni pamoja na maandalizi ya kutoa malazi kwa mazuwari wa Arbaeen.

Alisema maeneo 26 kwenye haram hiyo na kwingineko huko Najaf yametayarishwa kwa ajili ya malazi, ikiwa ni pamoja na eneo la Hazrat Zahra (SA) lenye uwezo wa kupokea wafanyaziara 30,000.

Rahim aliongeza kuwa vituo 10 vitatoa huduma za chakula huku vituo vingine kumi vikitoa huduma za afya na matibabu.

Kwa mujibu wa afisa huyo, pia kumekuwa na uratibu mzuri na makamanda wa usalama na polisi mjini Najaf na waziri wa mambo ya ndani wa Iraq ili kuhakikisha usalama wakati wa mjumuiko adhimu wa Arbaeen.

Wakati huo huo, Sheikh Ali Mouhan, afisa wa Haram Takarifu ya Hadhrat Abbas (AS), alisema idara ya masuala ya kidini haram hiyo itaweka vituo vya uenezaji kwenye njia ya mahujaji wa maandamano ya Arbaeen.

Alisema vipeperushi na vijitabu pia vimetayarishwa ambavyo vinajumuisha maswali na majibu juu ya maswala ya kidini, maamuzi ya kidini, na maswala kama walipaji, Hijabu, n.k.

Arbaeen ni neno la Kiarabu ambalo maana yake ni 40.  Katika muktadha huu, ni siku ya 40 tangu maadhimisho ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) na masahaba wake watiifu tarehe 10 Muharram katika siku ya Ashura. Mtukufu huyo aliuawa shahidi katika mapambano ya Karbala  karne 14 zilizopita.

Siku ya Imam Hussein (AS) ya Arbaeen inakuja tarehe 20 Safar, mwezi wa pili wa kalenda ya mwandamo wa Kiislamu.

Baada ya kufa shahidi Imam Hussein (AS) mikononi mwa katili Yazid bin Muawiya, watu ambao walishangazwa na ukatili wa ukoo wa Ummaya walianza kuzuru kaburi lake kutoa heshima zao na tokea wakati huo hadi leo vizazi katika umma wa Kiislamu vimeendeleza utaratibu huo. Kila mwaka idadi ya wafanyaziara katika Siku ya Arabeen inaongezeka ambapo mwaka uliopita idadi hiyo ilivunja rekodi na kufika milioni 21.

4164102

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen karbala najaf
captcha