IQNA

Uislamu unaenea kwa kasi

Bondia Maarufu Gervonta Davis asilimu katika Msikiti wa Maryland

20:49 - December 29, 2023
Habari ID: 3478108
IQNA - Gervonta Davis, bondia bingwa wa dunia kutoka Baltimore, Marekani alisilimu siku ya Jumapili katika msikiti mmoja. Hayo yamedokezwa na Sheikh Hassan Abdi, ambaye aliongoza sherehe hiyo.

Davis, ambaye alichukua jina la Kiislamu Abdul Wahid, linalomaanisha "Mtumishi wa Mmoja," alijiunga na Uislamu baada ya mazungumzo ya saa moja na Sheikh Abdi kuhusu kuwa mwanadamu bora.

Davis, 29, hajashindwa akiwa ameshinda mara 29 na ameshikilia taji la World Boxing Association (WBA) uzani mwepesi tangu 2019. Pia anajihusisha na miradi ya maendeleo ya jamii katika mji aliozaliwa, kama vile kukarabati nyumba huko Sandtown-Winchester, kitongoji cha West Baltimore alikokulia..

Sheikh Abdi, ambaye yuko Philadelphia na amehubiri kote Marekanii, alikutana na Davis na timu yake kwa kifungua kinywa baada ya kutambulishwa na Sabur Carter, msimamizi wa Masjid Al-Hidaayah huko Woodlawn, ambapo alisilimu. Sheikh Abdi alisema alishangazwa na unyenyekevu wa Davis.

Siku ya Jumatano, Davis alitembelea Tawheed First Academy, shule ya Waislamu huko Woodlawn, ili kujifunza zaidi kuhusu historia ya Uislamu Aliketi kwenye darasa la masomo ya Kiislamu na kuwatazama wanafunzi.

Davis hajabadilisha jina lake kisheria, jambo ambalo si wajibu wa kidini kwa wanaosilimu. Hata hivyo, baadhi ya watu maarufu waliosilimu wamefanya hivyo, kama vile bondia mashuhuri Cassius Clay, ambaye 

3486600

Kishikizo: bondia asilimu marekani
captcha